Na Luteni Selemani Semunyu

JAJI Mkuu wa Tanzania Mh Othman Chande anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Generali Geogre Waitara maarufu Waitara Trophy 2016.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wanaoandaa mashindano hayo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam.

Brigedia Jenerali Luwongo alisema maandalizi yamekamilika na yanatarajiwa kufanyika Jumamosi Novemba 19 na kushirikisha Wachezaji wa makundi yote isipokuwa watoto huku klabu zote zikithibitisha kushiriki.

“Tumeshajiandaa vya kutosha na wadhamini wametuwezesha na mwitikio mpaka sasa ni mkubwa na tayari wachezaji 150 wametibitisha kushiriki mashindano haya yanayodhaminiwa na kampuni ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha John Walker red label” Alisema Generali Luwongo.

Aliongeza kuwa mbali na Vilabu wenyeji klabu ya Lugalo ,Gymkhana Dar es Salaam,Gymkhana Morogoro ,Gymkhana Arusha, Kili,na TPC Moshi ,na Mufindi pia kutoka Arusha Mkuu wa majeshi Mstaafu Mirisho Sarakikya amethibitisha  kushiriki katika mashindano hayo.

Pia alisema Wanatarajia kuongea na Chama cha Golf Nchini ili kuona namna gani baadhi ya Mashindano ya Ndani ikiwemo hili la Waitara kuwa na hadhi ya Kimataifa kutokana na kuwa mashindano hayo na hamasa kubwa iliyopo.

Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kapten Japhet Masai alisema  mashindano hayo yatakuwa ya Stroke play Net ambapo yatatanguliwa na Wachezaji wa Kulipwa na Wachezaji wasaidizi siku ya Ijumaa Novemba 18 huku siku inayofuata yakifanyika kwa makundi yaliyosalia.

Naye Meneja wa mawasiliano wa Serengeti Abbas Abraham alisema maandalizi ya zawadi ikiwemo ya Vikombe yamekamilika na wanachosubiri ni zoezi la kukabidhiwa kwa Washindi.

Mashindano ya Kombe la Waitara yanayofanyika kila mwaka  ikiwa ni kumbukumbu ya kutambua mchango mkubwa uliotolewa na mkuu huyo wa majeshi katika kuanzisha Uwanja wa Golf wa Lugalo Mwaka 2006.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...