Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili
kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya
chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii
za awali.
Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya
Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii
(B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science)
wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190.(PICHA ZOTE NA
RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (hayupo
pichani) kuwatunuku digrii ya awali ya elimu ya jamii na ualimu wakati
wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo jioni. Jumla ya wanafunzi 864
walitunukiwa digrii hiyo.
Makamu Mkuu wa UDSM, akifurahi wakti wimbo wa kabila la wahaya wa Akanana Kalile Kona ukipigwa wakati wa mahafali hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...