Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.
Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190.
Wahitimu wa digrii ya awali ya elimu ya jamii na ualimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho jana jioni. Jumla ya wanafunzi 864 walitunukiwa digrii hiyo.
Mhitimu Bora wa Kike akipatiwa zawadi
Warda Jumanne akipatiwa zawadi ya kuwa mmoja wa wanafunzi Bora wa Kike. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...