Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MWILI  wa aliyekuwa Waziri  Mwandamizi Mstaafu Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa kesho katika Viwanja vya Karimjee majira ya saa tano asubuhi  na kisha kusafirishwa kuelekea Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kwa ajili ya mazishi.

Mungai  aliyezaliwa Oktoba 24,1943 alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi  aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa kipindi cha  miaka 35 na kufanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za utawala wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu ya pili, tatu .

Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni uwaziri wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mwanasiasa mkongwe Chrisant Mzindakaya amesema kuwa wataendelea kumkumbuka Mungai kwani moja ya wanasiasa waliokuwa na msimamo na aliweza kufanya mageuzi katika wizara alizokuwa anafanyia kazi  hususani wizara ya Kilimo na pia hakuwa na kusubiri kesho kama kuna jambo analoweza kulifanya leo hawezi kusubiri kesho.

Mtoto wa tatu wa marehemu,William Mungai amesema kuwa baada ya utaratibu wa kuaga mwili wa marehemu pale Karimjee watasafiri kuelekea Mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi yanayitarajiwa kufanyika Jumamosi majira ya saa nane mchana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...