Na Masanja Mabula -Pemba .

Jumla ya mikarafuu 173 katika mashamba ya Kichunjuu wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba inakisiwa kuwa imeteketea kwa moto uliyopelekea wanakijiji, sheha na mkuu wa misitu wawilaya kujitokeza kusaidiana kuuzima moto huo uliyokua unaendelea kuwaka.

Taarifa zinasema kua moto huo ulianza kuwaka tokea juzi majira ya saa 12 za jioni ambapo wananchi waliyojitokeza kuuzima bila ya kutambuakua upo baadhi yao hawakuuzima vizuri na hatimae kuendelea kuwaka mpaka siku ya pili.

Mmoja miongoni mwa wanakijiji hicho ndg: Kassim Juma Abdalla amesema tukio hilo ni la kusikitisha na kwa kukisia mashamba yaliyoteketea kwa moto huo ni mashamba sita.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi sheha wa shehia ya Mizingani Bw:Rajab Mbwana Rashid amethibithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kua, taarifa ya awali aliipata kupitia jeshi la polisi ambao walimpigia simu na kumtaarifu juu ya uwepo wa tukio hilo.

Amesema mara baada ya kupata taarifa hiyo alikwenda moja kwa moja katika eneo la tukio na kushuhudia uwepo wa moto huo huku ukiendelea kuteketeza mikarafuu iliyokuwamo katika mashamba hayo, hivyo kwa pamoja akiwemo mkuu wa misitu walaya kuuzima ili kunusuru majanga zaidi.

“kama ulivyokuona kule kulivyo, tulitaka tuwaite fire lakini wasingeweza kufika hivyo tukaamua tuuzime wenyewe” alisema sheha huyo.Akijibu suala la mwandishi wa habari hizi aliyetaka kufahamu nani waliyohusika kuuwasha moto huo pamoja na sababu iliyowafanya kufanya hivyo, sheha huyo amesema kuampaka muda huu bado hawajafahamu nani wahusika wala sababu yakufanya hivyo na kwakushirikiana na jeshi la polisi mkoa wanaendelea na uchunguzi ili kubaini halihalisi ya tukio hilo.

Akizungumzia wamiliki wa mashamba hayo, amesema kua bado hawajakutana na kufanya mazumzo ila jitihada hizo zipo ili kujua kitu katika tukio hilo.Kwa mujibu wa wakadiriaji wa mazao kutoka ZSTC, mikarafuu hiyo kwa mwaka inauwezo wa kuzalisha kilo 1160 sawa na gunia 23 yakiwa na thamani ya shilingi milioni kumi na sita laki mbili na arubaini elfu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...