THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

JUNDOKAN SO HONBU TANZANIA YAZIDI KUIMARIKA CHINI YA SENSEI RUMADHA FUNDI

Mtindo wa Karate wa Okinawa Goju Ryu shina la Jundokan So Honbu Tanzania linalo ongozwa na mkufunzi wake mwakilishi sensei Rumadha Fundi, kwa ushirikiano na uongozi wa dojo zote mbili, yaani Jamhuri na Zanaki  linazidi kuwa imara chini ya uongozi wa wakilishi wa matawi makuu mawili ya mtindo huo wa Goju Ryu.

Ingawa ni dojo au shule mbili, lakini zote zina lengo moja tu kulitumikia jamii ya wana Goju Ryu Karate. Sensei Rumadha, alipata fursa yakuwa na mazoezi na shule hizi mbili na pia kuafikiana na wanafunzi waandamizi wa shule hizo na kuleta mabadiliko katika mbinu za ufundishaji, ikiwa pamoja na kushirikiana kwa mazoezi ya pamoja mara kwa mara kati ya dojo hizo.
Jundokan Zanaki Dojo.

Mtindo huu wa Okinawa Giju Ryu, uliletwa hapa nchini na mwasisi wa mtindo huu, Sensei Nantambu Camara Bomani mwaka 1973, na  unaendelea kufundisha maadili, nidhamu  na mbinu  za kujilinda kama jinsi inavyo fundishwa kiasilia hivi sasa huko  Okinawa, Japan.

Sensei Rumadha pia, ameleza kujitolea kutoa mchango wake katika shule hizo, ikiwa na kuzitembelea mara moja kila mwaka na kuwa na semina ikiwemo kufanya majaribio au “Mitihani” ya mikanda ya ngazi za juu na vilevile mafunzo ya utafiti utumiaji kata au “Bunkai” kwa wanafunzi wa ngazi ya kati na  ya juu.

Sensei Rumadha alikaririwa akisema,  alipokelewa kwa ukarimu na unyenyekevu katika dojo zote mbili na wanafunzi waandamizi  na walimu pia. Senpai Yusuf Kimvuli, Senpai Abdul Waheed, Senpai Bilal, Senpai  Mwinyimvua, Sensei Maulid Pambwe, Sensei Mwagala chini ya Jamhuri dojo, pia kwa upande wa Zanaki Sensei Melkia, Sensei Rashid Almas, Senpai Seif, na uongozi wote wa Zanaki dojo akiwemo Mohammed Murudker.
Jundokan Jamhuri Dojo

Mipango ipo njiani kujadili na kupendekeza wanafunzi watakao fanya mitihani ya mikanda mieusi mwakani baada ya idhini ya Kancho Yoshihiro Miyazato toka makao makuu ya mtindo huo huko Naha, Okinawa.

Mara tu baada ya mkufunzi mkuu wa Jundokan Tanzania, Sensei Rumadha Fundi atakapo hudhuria Kongamano”Jundokan European Gasshuku 2017 ”  la kila mwaka mtindo wa Goju Ryu Jundokan So Honbu, utakao fanyika mjini Warsaw, Poland  mwezi July na kupata ushauri toka kwa viongozi watakao kuja toka Okinawa, Japan akiwemo mwenye kiti wa chama hicho  Kancho Yoshihiro Miyazato na washauri wake wakuu wa mbinu za juu wa Jundokan, Sensei  Tetsu Gima na Sensei Tsuneo Kinjo.

Tanzania ni moja ya nchi pekee katika Afrika mashariki yenye wana Karate wa mtindo wa Goju Ryu wenye uzoefu wa mafunzo ya Karate kwa miaka mingi.
Sensei Rumadha na masenpai Waheed kushoto na senpai Yusuf Kimvuli .
Uongozi wa Jundokan Jamhuri Dojo na bendera yao toka Naha, Okinawa , Japan .