Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga akisalimiana na Baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dar es Salaam alipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo leo Novemba 30, 2016. 
 Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga wakiangalia moja ya eneo la Gereza Segerea ambalo litajengwa nyumba za kuishi za Maafisa na askari wa Jeshi hilo(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kuu Segerea, ACP.  Godfrey Kavishe akiwaonesha eneo hilo walipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya Jeshi ambapo tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
 Moja ya eneo litakalojengwa nyumba za Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza lililopo katika eneo la Gereza Kuu Segerea, Jijini Dar es Salaam kama linavyoonekana katika picha.
 Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo waliopo katika Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam wakitembelea maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za watumishi wa Jeshi hilo. 
Moja ya nyumba ya mabati iliyopo katika Gereza la Mahabusu Keko kama inavyoonekana katika picha. Katika kukabiliana na uhaba wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Rais JPM aonyesha urais shupavu na shujaa.
    Rais JPM afanya majeshi yawe sawa kwani yote huenda vitani.
    Lakini rais JPM uwakumbuke nao kwenye kamisheni.
    Pia rais JPM uwakumbuke kwenye mishahara.
    Unification katika kozi ya awali. Gharama lakini imara, hakuna cha bure, dezo inaua.

    Ombi: kozi ya recruit ya kuwa private iwe kwa majeshi yoote bila kujali. hii itaongeza uwezo wa kushinda vita. Vita ya uganda ilitumia muda mrefu na vifo vya wapiganaji vilikuwa vingi kwa sababu askari wa majeshi yasiyo JW hawakuwa fiti saana kwa sababu ya kutofautisha mafunzo ya awali wakati wakati JW wenyewe wachache hawahkutosha. Risasi hauchagui askari lakini askari mwenye mafunzo sahihi atalenta ushindi na kuepuka vifo na majeruhi wasiyo lazima. Azma yako uliyosema nimekusapoti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...