NA RABI HUME.

KAMPUNI ya Paraa Mwanga ambayo inajihusisha na uuzaji wa sola imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la Tunaangaza Afrika ambayo itawawezesha watanzania kushiriki na kushinda kwa kutumia 500 tu.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela Krishnamurthy alisema malengo ya kampuni yao ni kusaidia maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme na hivyo kupitia kampeni hiyo wananchi watakuwa wakishiriki na kushinda zawadi ya sola za kampuni hiyo ambazo zitawasaidia kupata mwanga katika nyumba zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela Krishnamurthy akielezea kampeni ambayo wameanzisha itakayowawezesha watanzania kushinda vifaa vya umeme wa jua (sola) vinavyouzwa na kampuni hiyo.

“Kutakuwa na droo na itafanyika kila wiki na kutakuwa na mshindi, atakuwa akipatiwa tv na tutakuwa tunampatia sola, kila wiki atakuwa anatangazwa mshindi mmoja hadi shindano limalizike,” alisema Krishnamurthy.

Nae Meneja wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Michael Mbughi amezungumza kuhusu kampuni hiyo na kusema kuwa ni kampuni mpya Afrika ambayo kwa kuanza imeanzia Tanzania ili kuwezesha jamii ya watanzania na zaidi maeneo ya vijijini kupata vifaa vya umeme ambavyo vinauzwa na kampuni hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Michael Mbughi akizungumza kuhusu kampuni hiyo na bidhaa inazoziuza katika maeneo ambayo wanafanya kazi.

“Tuna mradi ulio na lengo la kuiangaza Afrika na hasa maeneo ya vijijini ambapo umeme haujafika, tumeona tuanzie Tanzania na baadae tutaenda katika nchi nyingine, na katika hilo tayari tumeenda Mbagala na kugawa bure sola katika kaya 10,

“Tutatuma watu wetu na baadae tutakuwa na mawakala katika mikoa ambayo tutakuwa tunafanya kazi, bidhaa hizi zipo za aina tofautitofauti na kwa kuanza tutakuwa katika mikoa na Kagera, Katavi, Sumbawanga na Rukwa,” alisema Mbughi.



Mmoja wa wafaidika wa msaada wa sola kutoka kampuni ya Paraa Mwanga, Said Athman akiwasha taa baada ya kuunganishiwa umeme huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...