Kampuni ya Shell pamoja na washirika wake, Pavilion Energy na Ophir Energy, wametangaza kuanza rasmi shughuli za  uchorongaji wa Visima vya utafiti wa gesi asilia  kwenye visima  viwili  ndani ya  vitalu namba 1 na namba 4  vilivyoko kina kirefu cha maji, katika  mwambao wa Mafia  na Mtwara.

Kazi hii ya utafiti itafanywa kweye kina cha maji marefu takribani mita 2,300 chini ya bahari.  Uchimbaji huu utafanywa na meli ijulikanayo kwa jina la “Noble Globe Trotter 2’’. Shuguli hii ya utafiti inatarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2016 na kumaliza mwanzoni mwa mwezi wa Januari 2017.

Shell Pamoja na washirika wake wanatarajia kuwekeza takribani Dola za kimarekani 80 milioni kwa ajili ya kufanya utafiti huu. Mwezi Februari 2016, Kampuni ya Shell iliungana na Kampuni ya BG group. Shell inaendesha shughuli zote za utafiti kwenye vitalu namba 1 na namba 4 kwa niaba ya washirika wengine. Aidha, katika shughuli zote za utafiti Kampuni ya Shell inafanya kazi kwa karibu na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC).

Sera ya Nishati na Madini ya  Taifa, pamoja na Dira ya Maendeleo ya  2025, vimeainisha umuhimu wa mradi wa kuchimba, kuchakata na kusindika gesi (LNG) na mikondo yake yote, Mkondo wa juu (upstream) na Mkondo wa chini (downstream). Utekelezaji wa miradi hii utaenda sambamba na mikakati ya kuongeza ugavi wa gesi asilia kwenye masoko ya ndani ya nchi.

Licha ya changamoto za kushuka kwa bei ya mafuta na gesi duniani, Shell pamoja na washirika wake wanaendelea kuangalia njia mbadala za kuendeleza mradi huu. Ili kufanikisha shughuli zote na hatimaye kuwa na mradi ambao ni endelevu, ushirikiano na mchango wa Serikali  ni wa muhimu  sana katika kipindi hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...