THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KINGBLEZ AACHANA NA BENDI YA FM ACADEMIA,ASAINI MKATABA WA MIAKA MITANO BENDI MPYA YA EAST AFRICAN GWASUMA MUSIC BANDI YA JIJINI ARUSHA

Na Woinde Shizza,Arusha

WASANII mbalimbali jijini hapa wanatarajiwa kuanza kupata neema ya kukuza vipaji vyao baada ya bendi mpya ya muziki kuanzishwa.

Bendi hiyo mpya 'East African ngwasuma music band itakuwa ikifanya kazi zake jijini hapa,ambapo Mkurugenzi wa bendi hiyo ya East African Ngwasuma Music bendi Mukhtar Abdul Bolydo (Obama) alisema ni fursa kwa vijana wenye vipaji vya sanaa ya muziki katika uimbaji kujitokeza ili kuwania nafasi katika bendi hiyo.

"Hivi sasa tumeanzisha bendi hii bado tunauhitaji wa vijana wasiopungua 20 kwani malengo yetu ni kuwa na bendi mbili hapo baadaye na ni wakati wa Arusha kupata burudani ya aina yake",alisema Abdul.

Alisema bendi hiyo itaongozwa na msanii nguli wa muziki kutoka Fm Academia ambaye amehama na kujiunga na bendi hiyo mpya kwa kiasi cha shilingi Milioni 20 na amesaini mkataba wa miaka mitano wa utoaji wa huduma ya muziki.

Msanii huyo 'King of the king'king'(mzee wa mujini) Kingombe Mohammed alisema ataitumikia bandi hiyo kwa ajili ya kutoa burudani."Nimekuwa FM Academia kwa miaka mingi hivi sasa nimehama na tumeamua kuanzisha bendi mpya itakayokuwa moto wa burudani,".alisema Mohammed.

Bendi hiyo mpya ya East African Ngwasuma Music bendi yenye makao yake makuu jijini hapa, ina jumla ya wasanii 12 kati yao wawili wanawake na kila msanii ana mkataba wa miaka miwili na baada ya hapo kama atafanya vizuri ataendelea kutumikia kulingana na uwezo wake.
Picha ikionyesha wa kwanza kushoto mwimbaji wa zamani wa bendi ya FM academia Kingombe Mohamed (kingblez) akisaini mkataba wa miaka mitano wa kufanya kazi katika bendi mpya ya East African Gwasuma music band iliyopo jijini Arusha, anayefuata wa kwanza kulia ni wakili wa bendi hiyo Vivianus Rugakingira,kwanza ni mkurugenzi wa bendi hiyo Muktar Abdu Bolydo (Obama) na wafanyakazi wake wakishuhudia king blez akisaini mkataba wa kufanyakazi katika bendi hiyo kwa miaka mitano .
Mkurugenzi wa bendi hiyo ya East African Ngwasuma Music bendi Mukhtar Abdul Bolydo (Obama) akisaini mkataba wa kumuajiri kingblez kwa muda wa mika mitano ambapo alisema amemchukuwa fm Academia kwa kiasi cha shilingi milioni 20 
 Afisa utamaduni wa jiji la Arusha Benson Maneno akimkabidhi KIng blez mkatabawake mara baada ya kusaini