THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KIOTA KIPYA CHA MARAHA NA BENDI MPYA YA MJENGONI VYAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA

Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni Bendi imezinduliwa rasmi mkoani Arusha,  huku ikiwaahidi mema wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia ndani ya jiji hilo .

Akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi rasmi wa bendi hiyo Rais wa bendi Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa wamejipanga kufanya mkoa wa Arusha kuwa na bendi kubwa inayotoa burudani ya nguvu kama zilivyo bandi zingine za jiji la Dar es salaam akatolea mfano FM Academia na malaika bendi.

Alisema kuwa wakazi wa mikoani wamekuwa wakitegemea bendi kutoka jijini dar lakini kwa sasa ivi wamesogezewa burudani karibu kabisa na itakuwa kila siku za wekendi

Aidha alibaiisha kuwa bendi hiyo anayoisimania inawanamziki wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu pamoja na uzoefu wakutosha ivyo anaamini wapenzi wa mziki wa dance wataipenda bendi hiyo na kuikubali

Alisema adi sasa bendi na inanyimbo zake na wanajipanga kwa ajili ya kurekodi ili wapenzi ,wadau na wananchi waweze kupata mziki na kuhusikia katika maredio na hata wanapokuwa majumbani.

Alimalizia kwakusema kuwa bendi hiyo ya mjengoni itakuwa inatoa burudani kila wekendi hivyo wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia wajitokeze kuja kupata burudani ya nguvu inayotoka kwa wanamuziki wa bendi hiyo.Kwa upande wake wa mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John mdeme alisema kuwa ameamua kufungua kiota ichikipya ili wakazi wa jiji la arusha wawez e kupata sehemu ya kistaarabu ya kupata chakula ,nyama choma nzuri pamoja na mziki mzuri wa live bandi

Alisema kuwa kimepita kipindi kirefu wakazi wa jiji la Arusha wamekuwa wanakosa sehemu ya kwenda kupata burudani nzuri ya mziki wa bakurutu pamoja na live bendi inayoeleweka tangu hotel ya sabasaba ifungwe ivyo ameamua kuileta burudani hiyo ili wananchi wa Arusha waweze kupata sehemu ya kustarehe.


Alimewakaribisha wageni kutoka mikoani pindi wanapofika jijini Arusha kutoaacha kuja mjengoni kujipatia burudani ya nguvu kutoka katika bendi ya mjengoni pamoja na nyama choma nzuri na freshi inayotengenezwa na wachoma nyama waliobobea katika sekta hiyo.

Mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni kabu pamoja na mjengoni band wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza).
Bendi mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo .Habari picha na Woinde Shizza,wa libeneke la kaskazini blog