Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii .
Jumuiya ya watu wa China iliyopo Tanzania imeandaa Maonesho ya Kimataifa kwa ajili ya kuimarisha utamaduni wa kati ya Tanzania na China ambayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 12 hadi 24 mwaka huu katika Kituo cha Utamaduni wa nchi hiyo.


Maonesho hayo ni kuwafanya watanzania kuwa kitu kimoja kutokana na mahusiano ya miaka mingi na kuendelea kukua kila siku.


Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa China Nchini Tanzania Liu Jing pamoja na Mgeni rasmi katika maonesho hayo ni Balozi wa china , pamoja na Waziri mkuu wa Habari, sanaa utamaduni na Michezo Nape Nauye 

Akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni wa Ubalozi wa China Nchini, Gao Wei amesema kuwa maonyesho hayo yatambatana na kumbukumbu ya miaka 400 ya William Shakespear na Tang Xianzu ambaye alikuwa mwandishi wa Riwaya na Tamthilia za kichina kwa lengo la kutambua mchango wao kwa kutangaza tamaduni za kichina kwa kupitia vitabu na tamthilia.

Ameongeza kuwa Tang Xianzu ambaye amezaliwa mwaka 1550 aliweza kupigania utamaduni wa kichina baada ya kuchoshwa na maisha ya kwao na kufanikiwa kuandika mashairi 2000 mnamo mwaka 1598, pia atakumbukwa kupitia Tamthilia zake kama, The Peony Pavilion,The Puple hairpin, Record of the Southern Bough na Record of Handan, ambavyo kwa pamoja vilijulikana kama ndoto za Linchuan.

Maonesho hayo pia yataonyesha vitu tofauti katika maisha kwa kutumia sanaa ambayo itahamasisha jamii ya wachina na jamii nyingine na kuwafanya wageni kuelewa usawa na tofauti iliyopo kati ya utamaduni wa maisha ya nchi za Magharibi na Mashariki.
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni wa Ubalozi wa China Nchini, Gao Wei

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...