Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi mapema leo ameongoza zoezi lakuteketeza bidhaa mbali mbali yakiwamo Madawa ya Binadamu (Drip, Dawa za maumivu), Vyakula, Vipodozi nk...

DC ametekeleza zoezi hilo baada yakuwa amewaagiza watu wa TFDA, kufanya Msako Madukani kuangalia ubora wa Bidhaa.

Ndejembi akizungumza mapema alisema "Niliagiza watu wa TFDA kufanya msako wa Bidhaa zilizokwisha muda wake, Lengo langu nikuhakikisha Kongwa haiwi Kichaka cha Bidhaa zilizokwisha muda wake".

akiwa na Kamati yake ya ulinzi na Usalama Wamesema kuwa Zoezi hilo ni Endelevu ili kukomesha ujanja ujanja wa Wafanya Biashara wasio na Maadili mema ya ufanyaji Biashara.
Sehemu ya Bidhaa hizo zikiwa zimetupwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akiwa na Kamati yake ya Ulinzi la Usalama pamoja na Maafisa wa TFDA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wiki moja kabla mngeweza hata kuwapa wagonjwa hospitalini hata kwa nusu bei, au wanafunzi wa mabwenini, wafungwa magerezani, watu masikini ombaomba. Mmeacha tu mpaka tarehe ipite mharibu chakula wakati kuna watu wanalala njaa.

    Mdau uarabuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...