SABINUS       PETER      KWEKA
30/12/ 1935  - 22/11/2004

       Baba yetu mpendwa, leo umetimiza miaka kumi na mbili (12) tokea siku ulipotuacha gafla bila ya kwaheri kutokana na shinikizo la Damu (Stroke). Hatuna cha kusema ila tunabaki kushukuru tuu maana ilimpendeza Bwana zaidi.
        Baba, tunakukumbuka sana na bado tunahuzunika hasa tunapokumbuka mapokezi yako ya upendo tulipokuwa tukija nyumbani, ulitupenda sana hilo tunakiri ulipenda hata majirani waliokuzunguka, ukiwapa ushauri na misaada mingi hata wakakuchagua kuwa Diwani wao na M/Kiti wa Kanisa. Ulimpenda sana Mungu, hatukulala wala kuamka bila ya kuomba Rozari ilikuwa nguzo yako kuu.
Ulipenda sana Elimu, ulipiga vita sana adui ujinga kwa nguvu zako zote,ulitusomesha pamoja mshahara wako ulikuwa mdogo, tunatamani sana ungekuwepo ufaidi hata matunda ya jasho lako hilo. Ulipenda sana tujue njia mbadala  za kupata kipato kingine kama Kilimo, n.k. Maana ulisema mshahara tuu si kitu. Ulitufundisha biashara ili tukikwama makazini tujue pa kukimbilia kweli ulikuwa Baba mfano mzuri wa kuigwa.
Unakumbukwa sana na sisi wanao JANE, FESTO,EUGENIA,ELIZABETH, CECILIA  na THADEI, WAJUKUU NA VITUKUU, dadako wa pekee SR. DEVOTHA KWEKA CDNK, WAKWEKA wote wa NARUMU, Ndugu, na Marafiki wote.
Misa ya kumuombea imefanyika leo Parokia ya Mkolani.
“Raha ya Milele Umpe Eee Bwana…..”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...