Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa shukrani kwa madaktari bingwa walioletwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Munadhammat Aldaawa kwa kushirikiana na Ubalizi wa Tanzania nchini Saudi Arabia chini ya ufadhili wa Umoja wa Vijana wa Kiislamu duniani (WAMY) baada ya kumaliza kutoa huduma za matibabu kwa muda wa siku 10 kisiwani Pemba.
Mkurugenzi wa Munadhamat Aldawa Al islamia Tanzania Dkt. Khalid Al-Awadh akimueleza Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo huduma walizotoa kisiwani Pemba kwa muda wa siku 10, (katikati) Mratibu wa WAMY nchini Saudiarabia Dkt. Ibrahim Algamaan.
Baadhi ya madaktari waliokuwa wakitoa huduma za afya Kisiwani Pemba kutoka Jumuiya ya Munadhamat wakiwa katika mkutano na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayup pichani) Ofisini kwake Mnazimmoja.
Mratibu wa WAMY Dkt. Ibrahim Algamaan akiwa na madaktari wenzake akimkabidhi zawadi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kama ukumbusho wao kwake walipokwenda kuonana nae ofisini kwake Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...