Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Mhe Joseph Mkirikiti amehimiza uzalishaji wa mafuta ya Alizeti, Ufuta na Nazi kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa sababu ni kioo na msingi imara ya kuwawezesha ajira iwe ya kudumu na tena ajira bora kwa wananchi. 

Hayo aliyasema akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa vitendo kwa wakulima ambao ni wazalishaji wa bidhaa za mbegu za mafuta ya ufuta, nazi na alizeti wa Ruangwa na akipokea lebo za vifungashio vya mafuta ya alizeti kwa wazalishaji wa bidhaa za mafuta ya alizeti zaidi ya 1000 zilizotengezwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

Mafunzo hayo yameanza tarehe 7 hadi 10 Novemba, 2016 juu ya namna ya ufungashaji bora wa bidhaa za mbegu za mafuta ya ufuta, alizeti na nazi, kuwa na lebo bora kwenye kila bidhaa inayozalishwa, rajamu (branding) kwenye bidhaa hizo, namna ya kuboresha ubora wa bidhaa na mbinu ya kuuza bidhaa hizo kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi kwa wazalishaji wapatao 50 wa Ruangwa na 50 wa Masasi.

“Elimu mtakayopata hapa itawachukueni kwenye hatua nyingine ya kufanya maboresho makubwa ya ajira yenu, hapa nchini mahitaji ya mafuta ya kula kwa mwaka ni lita 350,000 wakati uzalishaji kwa sasa ni asilimia 40 pekee na asilimia 60 huagizwa kutoka nje ya nchi hivyo basi, tuna fursa kubwa ya kunufaika na sekta hii.” 
Mhe Joseph Mkirikiti akikabidhi lebo za vifungashio kwa Bi Safina Selemani mzalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka kata ya Nandagala B kikundi cha CHIUKUTE, lebo hizo zimetengenezwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade)
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe Joseph Mkirikiti akipokea lebo za vifungashio kwa wazalishaji wa mafuta ya alizeti katika mkoa wa Ruangwa kata ya Nandagala B kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade) Bw Edwin Rutageruka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...