THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAJIBU YA SERIKALI YA HOJA ZA WABUNGE KUHUSU MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA MWONGOZO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/2018


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB), (kushoto), akijibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma

Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), baada ya kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuwasilisha kwa umahili mkubwa majibu ya serikali kutokana na hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (kulia) pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Tume hiyo baada ya kuwasilishwa kwa majibu ya hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Kamisha wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Cheyo (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (katikati) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba, nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb), kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma. (Picha zote na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango)