Hussein Makame, NEC

Wahenga walisema “Safari bila ya dira huishia kupotea njia”. Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Tume ya Taifa ya uchaguzi iliamua Kufanya tathmini ili kubaini utekelezaji wa uchaguzi mkuu.Katika utekelezaji wa mkakati wowote ni muhimu kuwa na dira ili kujua mafanikio au kushindwa kwa utekelezaji wa mkakati huo.

Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilifanya tathmini ya Uchaguzi huo katika halmashauri 75 kwa kuwahoji na kujadiliana na wadau mbalimbali wa uchaguzi ili kupata mtazamo wao juu ya Uchaguzi huo.

Oktoba 28 mwaka huu, NEC imekabidhi Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama kwa niaba ya Serikali, kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva anasema Tathmini hiyo imefanyika kuanzia tarehe 1 hadi 26 mwezi Februari, 2016 katika Mikoa 22 kati ya mikoa 30 iliyokuwepo wakati wa Uchaguzi huo, Halmashauri 64 kati ya 181, Kata 192 kati ya 3,953 za Tanzania Bara na Shehia 12 kati ya 386 za Tanzania Zanzibar.
wenyekitiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhiWaziri wa Nchi Ofisi ya WaziriMkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na WalemavuMhe. JenistaMuhagama (kulia) Taarifa ya TathminiBaada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwaniwamwaka 2015, mjini Dodoma.
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuva (kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya WaziriMkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na WalemavuMhe. JenistaMuhagama, wakioneshaVitabu vya Taarifa ya TathminiBaada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwanimwaka 2015, mjini Dodoma.
Waziriwa Nchi Ofisi ya WaziriMkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na WalemavuMhe. JenistaMuhagamaakihutubiamkutano wa kukabidhi Taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwaniwamwaka 2015, mjini Dodoma.Kushoto niMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Damian Lubuvana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.Pichana Hussein Makame, NEC


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tathmini ni muhimu ila ilitakiwa afanywe na taasisi nyingine sio NEC inafanya tathmini ya kazi waliyoifanya wenyewe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...