Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeyakumbusha makampuni ya simu za mkononi hapa
nchini kukamilisha taratibu za kisheria za masoko ya mitaji na hisa kwa
kutoa asilimia 25 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ili
kuwawezesha wananchi kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa
kampuni.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa
Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa Kutolewa kwa hisa hizo kutawasaidia
watanzania wengi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hizo na pia kunufaika na gawio la kila mwaka.
“Tarehe
23 Juni, 2016, Bunge lilipitisha mswada wa sheria ya Fedha ya 2016
yaani the Finance Act 2016 pamoja na mambo mengine ulifanyia mabadiliko
Sheria ya electroniki na mawasiliano ya
posta,” alisema na kuongeza kuwa ambapo makapuni ya mawasiliano
yaliyoandikishwa kufanyabiashara hapa nchini kumilikisha asilimia 25 ya
hisa zake kwa umma kwa kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam ndani ya kipindi cha miezi sita.
Alisema
zaidi ya watanzania milioni 20 wanamiliki na kutumia simu za mikono
katika shughuli zao za kila siku na hivyo basi, wakati umefika kwao kama
wateja wa muda mrefu kuanza kunufaika kama sehemu ya wamiliki wa kampuni hizo kupitia hisa.
“Sisi
kama baraza, nachukua fursa hii kuwahimiza watanzania wote kujiandaa
kushiriki kikamilifu katika kununua hisa za makampuni hayo ya simu mara
yatakapokamilisha taratibu za kujiunga na soko la hisa la DSE,”Bi. Issa
alisisitiza.
Kwa
mujibu wa Katibu Mtendaji huyo, Baraza litatoa elimu kwa umma kwa muda
wa mwezi mmoja kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika kuelimisha na
kuhamasisha umma kuhusu fursa hiyo muhimu kiuchumi.
“Tunapenda
pia kutoa rai kwa mashirika ya Hifadhi ya Jamii nchini kuandaa
utaratibu mzuri utakaowawezesha wanachama wao kuweza kushiriki katika
kununua hisa za makapuni hayo ya simu mara yatakapojiunga na soko la
hisa,” alisema.
Aidha,
Bi. Issa alisema, Baraza linafuatilia kwa karibu sana maendeleo ya
utekelezaji wa mabadiliko hayo ya kisheria na kuhakikisha utekelezaji
wake unafanyika kwa wakati kama ilivyoainishwa kati sheria ya mwaka
2016.
Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi lipo chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu na linasimamia Mkakati wa Kitaifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
kupitia madawati ya uwezeshaji kuanzia ngazi ya Wizara,Idara, Taasisi,
Mikoa na Halmashauri zote nchini.
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’I Issa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana wakati akiyakumbusha makampuni ya simu za mkononi hapa nchini kukamilisha taratibu za kisheria za masoko ya mitaji na hisa kwa kutoa asilimia 25 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kuwawezesha wananchi kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Baraza hilo, Bw. Edward Kessy.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...