Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha rasilimali ya gesi na mafuta inakuwa ni chachu ya kukuza uchumi wa taifa na wa wananchi kwa ujumla.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo 22-Nov-2016 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya gesi na mafuta barani Afrika ulioandaliwa na Kampuni ya Getenergy ya Uingereza.

Katika hotuba yake, Makamu wa Rais amewahakikishia washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi na itakuwa bega kwa bega na wadau wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha uwekezaji utakaofanyika unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.




Amesisitiza kuwa kwa sasa Serikali ya Tanzania inaendelea na mkakati kabambe wa kusomesha wataalamu wa fani ya mafuta na gesi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa wataalamu hao ambao watakuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa katika sekta za gesi na mafuta.

Makamu wa Rais amesema Tanzania imegundua kiasi kikubwa na gesi na ana imani kubwa kuwa mafuta nayo yanapatikana hivyo ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kujipanga kuwa na wataalamu wake wazalendo wa kutosha watakaoshikiri katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanajihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa rasilimali ya gesi na mafuta zitakagundulika na kuchimbwa barani Afrika zitasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa mataifa hayo, uchumi ambao utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi katika nchi husika.

Mkutano huo wa siku Mbili wa Kimataifa umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya gesi na mafuta kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu kuhusu njia bora za uwekezaji katika sekta hiyo barani Afrika.

Kwa upande wake,Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kwa Serikali itaendelea kusomesha wataalamu wake ndani na nje ya nchi ili kujitosheleza kwa wataalamu wa sekta hiyo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza wataalamu wa masuala ya gesi kutoka Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wazalishaji Petroli Afrika, Mhandisi Mahaman Laouan Gaya mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam 
Wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan wakati wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...