THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUTENDA ILIYOAHIDI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi mkoa wa Mwanza kuimarisha maradufu doria katika Ziwa Victoria kama hatua ya kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu ambao umepunguza kwa kiasi kikubwa samaki kwenye ziwa hilo.

Makamu wa Rais ametoa maagiza hayo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika wilaya za Kwimba, Misungwi na Magu mkoani Mwanza katika ziara yake ya kikazi ambayo imeigia siku ya PILI mkoani humo.

Makamu wa Rais amewataka viongozi hao kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaokamatwa wakivua kwa zana haramu ua kwa sumu ili kukomesha tatizo hilo katika Ziwa Victoria.

Ameonya kuwa wavuvi haramu wakiachwa waendelee kufanya uvuvi huo wataharibu ziwa lote hasa mazalia ya samaki hali ambayo itasababisha viwanda wa kusindika samaki mkoani humo kufungwa na mamia ya watu kukosa ajira kutokana na shughuli za uvuvi.

Akizindua na kuweka mawe ya msingi kweye mabweni ya wanafunzi wasichana katika shule za sekondari ya Idetemya wilayani Misungwi na shule ya Sekondari ya Archbishop Anthony Mayala wilayani Kwimba, Makamu wa Rais amepongeza juhudi za viongozi wa mkoa wa Mwanza na wadau wa maendeleo kwa kujenga mabweni hayo ambayo yatasaidia wasichana kuondokana na mazingira hatarishi ikiwemo kupata mimba.

Makamu wa Rais amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuweka mikakati madhubuti ya kujenga mabweni ya wasichana kama hatua ya kukabiliana na tatizo la wanafunzi kupata mimba na kuacha shule.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Nsola ambapo alikagua miradi mbali mbali ya ufugaji samaki ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akikagua shamba la kilimo cha kisasa Greenhouse (Bandakitalu) la Ngongoseke lililopo kijiji cha Nsola wilayani Magu mkoa wa Mwanza 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimsikiliza kwa makini mwanafunzi Evodia Anatori wa shule ya sekondari ya kata ya Idetemya akionyesha kwa vitendo namna ya kuchanganya kemikali kwenye maabara ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi wa Idetemya mara baada ya kufungua bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye  maeneo ya Nyakato mkoani Mwanza.