Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa mwezi Mwezi Moja kuanzia leo tarehe 18-Nov-2016 kwa watendaji na viongozi waandamizi wa wilaya ya Ilemela wahamie kwenye wilaya hiyo haraka iwezekanavyo na waache tabia ya kukaa kwenye wilaya nyingine kwa kisingizio cha kukosa nyumba za serikali.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo katika hotuba yake kwa wananachi na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi jengo la utawala la Manispaa hiyo na kukabidhi madawati 1,074 yaliyotolewa na ofisi ya Bunge.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia hiyo na amewataka viongozi hao wahamie karibu na maeneo yao ya kazi kabla ya muda aliotoa kwisha ili waweze kuwa karibu na wananchi katika kuwasaidia kutatua kero na matatizo yanayowakabili kwa haraka.
2

Akiwa katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa mchinjio ya Nyakato jijini Mwanza, Makamu wa Rais ameuagiza uongozi jiji la Mwanza kusimamia kikamilifu mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato na watendaji watakaobainika kuhujumu mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni Tatu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa wananchi na watendaji wa jiji la Mwanza waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato unaohusisha uboreshaji wa jengo la machinjio,tanki la kuhifadhi maji,ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi nyama na ujenzi wa mtambo wa kutibu majitaka yanayotoka kwenye machinjio hiyo.

Makamu wa Rais katika hotuba yake, amesema hategemei hata kidogo ukarabati wa machinjio hiyo ufanyike chini ya kiwango kwa sababu ni mradi wa kibiashara ambao ukikamilika na kuanza kufanya kazi utasaidia jiji la Mwanza kupata mapato yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Makamu wa Rais pia amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ahakikishe anasimamia uundaji wa menejimenti ya machinjio hiyo ambayo itafanya kazi vizuri na sio kuingiza watu ambao hawana uwezo ambao watakwamisha utendaji kazi wa machinjio hiyo.

Kuhusu ukusanyaji wa kodi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia ya kielekroniki kutoka kwenye vyanzo mbalimbali fedha ambazo zitasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi mkoani humo.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wananchi nchini wahakikishe wanadai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali kwani kufanya hiyo watasaidia kuongeza mapato yake ambao yataelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wananchi wa Nyamagana kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa machinjio ya Nyamagana kutoka kwa Mhandisi wa jiji la Mwanza Ndugu Ezekiel Kunyalanyala (kushoto) kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya  Ilemela . 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akikikabidhi madawati kwa Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ambayo yalitolewa na Ofisi ya Bunge ambapo zaidi ya madawati 1074 yalikabidhiwa kwa wilaya ya Nyamagana na Ilemela. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua jengo la Manispaa ya Ilemela. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...