Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Paul Makonda amepiga marufuku biashara ya samaki kandokando ya barabara inayoelekea kivukoni na soko la samaki la feri baada ya wafanyabishara wa feri kulalamika kwa mkuu wa mkoa huyo kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakwepa kodi.

Awali Makonda aliambiwa na wafanyabiashara hao kuwa soko hilo linakosa wateja kutokana na kushindwa kufikiwa na wateja ambao hununua samaki au bidhaa nyengine kandokando ya barabara na kusababisha wateja kutofika sokoni humo.

Wakati huo huo Makonda amesikitishwa na kitendo cha wakuu wa idara mbalimbali kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati kwa kisingizo cha kutopata fedha za bajeti ya serikali kuu ikiwa wangeweza kubuni miradi itakayowaingizia fedha.

RC Makonda alisema kuwa hatakubaliana na watendaji wa namna hiyo kwani hurudisha maendeleo nyuma.

 Mnada wa samaki katika Soko la Feri ulipokuwa ukiendelea mapema jana jioni. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Anatoglo jana jijini Dar es salaam.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo akizungumza machache katika ukumbi wa Anatoglo jana jijini Dar es salaam.
 Viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala wakimsikiliza  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ukumbi wa Anatoglo jana  jijini Dar es salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...