Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasaa watumishi wa Umma wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) na kuacha kufikiria akistaafu atajenga nyumba sehemu zipi.

Makonda aliyasema hayo wakati alipotembelea miradi ya nyumba za watumishi wa umma za Bunju B pamoja na Magomeni Kota inayotekelezwa na TBA, amesema kuwa kujengwa kwa nyumba hizo kutafanya watumishi kufanya kazi kwa uhakika kutokana na mazingira ya kustaafu yamewekewa msingi na serikali ya kupatikana kwa nyumba.

Amesema watumishi wa umma wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mwingi wakifikiria nyumba kutokana na kipato chake hawezi kujenga nyumba hivyo kuwepo kwa nyumba zilizojengwa na TBA zitawaondolea machungu ya kufikiria suala la nyumba.

Aidha amesema kuwa Mradi wa Magomeni Kota ameshaanza kutekelezwa kutokana na ahadi aliyoitoa Rais Dk. John Magufuli kuona wananchi waliondolewa katika Kota hizo wananufaika na nyumba zitazojengwa.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga amesema kuwa watanzania wawaamini wamedhamiria kujenga kila mkoa kwa kuanzia nyumba 10 ili watumishi waweze kupata makazi.

Amesema kuwa ndani ya mwaka mmoja watakuwa wamemaliza mradi wa Ujenzi wa Magomeni Kota utakuwa umekamilika kutokana na kujipanga ili kuweza wananchi waanze kuishi katika nyumba hizo.

Mwakalinga amesema katika mradi wa Bunju B wametumika kati sh.Bilioni 13 hadi 14 katika kitalu cha 19 wameweza kujenga nyumba 219 na mradi mwingine watajenga nyumba 300 kwa viwango tofauti kutokana na vipato vya wafanyakazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua mradi nyumba zilizojengwa na TBA katika eneo la Bunju B katika ziara aliyoifanya leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga akimpa maelezo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda juu ya mradi wa nyumba za watumishi wa umma Bunju B leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga akizungumza na waandishi wa habari juu ya miradi inayotekelezwa na TBA ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...