THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Manyanya:Foundation sio sifa ya mtu kujiunga chuo kikuu

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi(Kushoto),Eng.Stella Manyanya akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Elimu,Prof.Simon Msanjila

Na Chalila Kibuda.

Kozi za foundation katika  vyuo  zinazotolewa sio mfumo wa Elimu uliopangwa na serikali kumfanya aliyepita kuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kozi za foundation  katika vyuo haijawekewa mfumo ambao unatambulika.

Mhandisi Stella amesema utaratibu  huo vyuo vimefanya vyenyewe hivyo serikali haiwezi kuukubali mfumo elimu hiyo.

Amesema anaesoma foundation apewe cheti na kama atahitaji  kujiendeleza asafishe cheti au asome mfumo ambao utamfikisha katika shahada.
Amesema suala la watu waliosoma cheti kisha diploma na wakajiunga chuo kikuu hawako sahihi kutokana na vyeti hivyo.Amesema serikali inafanya maboresho ya elimu nchini kutokana na kibaoni vitu vingi ambavyo vimetokana na watu kwenda tofauti na mfumo wa elimu uliowekwa.

Stella amesema wanaendelea kufanya maboresho katika diploma ya ualimu kuweza kuiondoa.Aidha amesema kuwa serikali haitaruhusu elimu kuwa holela kwa watu kuwa tofauti na mfumo uliowekwa.


Kuna Maoni 5 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Pelekeni muswada bungeni iwe sheria hata kama mtaondoka iendelee. la sivyo baada ya miaka 10 tutarudi kulekule kuwapa digrii wasiofaaa mpaka tunapata madaktari wa kuacha visu tumboni na wahandisi wa kuangusha magorofa.

 2. Anonymous Anasema:

  hata mimi ningekuwa waziri ningetenda hivyo. elimu haina dili wala uchochoro wala mbadala.

  Maprofessa wanaompinga Ndalichako nao hoi tuuu. Ndo hao walidahili darasa la watu 7000 UDOM. Wanapinga kwa sababu wana midomo.

  Ili tuinue elimu yetu ni lazima tuangalie quality assurance.

  Big up JPM & Ndalichako (mtawakoma viongozi wasomi wa kweli)

 3. Anonymous Anasema:

  anayetaka kwenda chuo kikuu asome form VI.

  aliyefli form VI arudie mpaka afaulu siyo kupiga dili.

 4. Anonymous Anasema:

  Mbona nafasi za kazi kama jeshi hamna dili? kwamba ambaye si mrefu akivaa stuli atadahiliwa jeshini pia?

 5. Anonymous Anasema:

  Form VI haina mbadala. Na waliopata digrii bila form VI wanyanganywe vyeti.