Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taasisi za Serikali kutekeleza agizo la kuhuisha taarifa na huduma katika Tovuti zao mapema kabla ya mwisho wa mwezi huu katika mkutano uliofanyika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.
Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao hivi karibuni jijini Dar es Salaam, kuhusu taasisi za umma kuhuisha taarifa katika Tovuti zao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akiwaonyesha waandishi wa habari mwongozo wa utengenezaji wa Tovuti za Serikali wakati wa mkutano wake na waandishi hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.

Na Ismail Ngayonga, Dar es Salaam.

SERA ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya mwaka 2003, pamoja na mambo mengine inasisitiza umuhimu wa  Serikali kutumia fursa za TEHAMA katika utendaji kazi wa kila siku na utoaji huduma kwa wananchi.

Katika kutekeleza sera hiyo, mwaka 2004 Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) ilianza kuchukua hatua mbalimbali kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kuimarisha mifumo ya utoaji habari na huduma kwa wananchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...