Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba dhidi ya Baraza la Wadhamini wa Chama hicho imeendelea tena katika mahakama kuu ya Tanzania kwa upande wa Mawakili wa mashtaka kuwasilisha ombi la kutokuwa na Imani na Jaji anaenendesha kesi hiyo.

Akizungumza wakati wa kuendesha kesi hiyo, Jaji Sakiati Kihiyo aliwataka watoa hoja kuja na hoja hiyo siku ambayo kesi imepangwa kusikilizwa Desemba 6 mwaka huu.

Jaji Kihiyo aliwataka upande wa mawakili wa baraza la wadhamini kusubiri barua  hiyo ya kumtaka ajiondoe kwenye kesi hiyo imfikie ndipo itakapo sikilizwa.
Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibraimu Lipumba, akitoka katika Mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Wafuasi wa Cuf wakipanda kwenye lori mara baada ya kutoka Mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...