Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Jamaa amelizungumzia hili suala kwa ufanisi saana. Hongera ndugu kwa kuweka wazi hili suala la kumiliki ardhi kwa wasio wa Tanzania.

    Sasa watu wajipange sio kupiga kelele tu.
    Tuwekee mtandao/Blog yako ili tufuatilie hili suala.

    Shukran.

    Mdau

    Maryland

    ReplyDelete
  2. Mdau kagusia mambo mengi ya muhimu, na haswa kukurupuka kwetu kwenye mitandao bila kuwa na facts!

    ReplyDelete
  3. Hili swala lilishakwisha na mapendekezo au uamuzi ulishatolewa na kuwekwa ktk rasimu ya katiba kwamba HAKUNA URAIA PACHA. Nakubariana na maamuzi yaliyofikiwa kwakua wadau waliopendekeza KUUKATAA muswada wa URAIA PACHA waliangalia pande zote na kupima hasara na faida. Kwakua hasara zilizidi uzito wa faida hivyo wakafikia maamuzi ya kuyakataa mapendekezo. Ukisikiliza maelezo ya msemaji ktk video amezungumzia suala la watu wa Diaspora kupoteza haki yao ya kumiliki ardhi na hasa ndio hoja yao kubwa japo pia amepitia mlango wa nyuma na kuzungumzia suala la uwekezaji ktk ardhi ya Tanzania kana kwamba watu wote wanaoishi nje wanamipesa ya kuwekeza bongo na kutoa ajira na hatimae kumaliza tatizo la ajira. Binafsi nashindwa kuwaelewa kwanini watu walikurupuka na kuukana uraia wa Tanzania na sasa wanalialia. Waafrika Waliowengi walikana na wanaendelea kukana uraia wa nchi zao kana kwamba wanajua kesho itakuaje na hawana sababu ya msingi ya kufanya maamuzi haya magumu ya kukana uraia wa nchi uliyozaliwa ,nchi ambayo baba na mama yako wamezaliwa wewe unakana tena kwa sababu nyepesi tu mfano eti ukisafiri usipate kero ktk viwanja vya ndege,najua wapo watakaosema walibadiri kwa sababu ya kusoma ili wapate msaada au usahisi wa ada, hili laweza kufanyika tena pasi na kuukana uraia wako.Nina jerani yangu hapa Sweden anatoka nchi jerani ya TZ pia kwa huko home, huyu bibie kaukana uraia wa nchi yake na kupata paspoti ya Swed, akaona haitoshi akaomba na paspoti ya umoja wa ulaya, akaona haitoshi akaomba na kibali cha Scandnavian countries lakini cha ajabu hajawahi kuvitumia hata siku moja vibali vyote alivyonavyo aina hii ya Waafrika ni wengi mno huku ughaibuni na ndio hao leo wanaotaka na paspoti ya Tanzania baadae hata hivyo viwanda hatutaviona zaidi ya kuianika nchi au kuiweka rehani nchi ktk mikono ya wasipenda kuiona ikisonga mbele. Mimi naishi hapa huu ni mwaka wa kumi natumia kibali cha kuishi cha kudumu abadani asilani sitoukana Utanzania wangu, alhamdulillah mambo yanakwenda vizuri. Kama ni kuwekeza wangemuuliza Dangote aliwezaje kwenda Ntwara hali ya kua si Mbongo??? Au Wachina wanaouza chemli na kupewa kibali cha uwekezaji mbona hawalilii Utanzania ili wafanye biashara zao tena ni za mama ntilie na kuuza maindi ya kuchoma.Namshauri msemaji badala ya kufikiria kuwakutanisha wanadiaspora online ingekua busara akawakutanisha hao wenye nia ya kuwekeza wakaenda home wakawekeza.Wangeanza na hili kwanza ili kujenga uaminifu na Serikali. Wasiwasi wangu ni kwamba wapo kweli wenye nia ya dhati na uwezo huo wa kuwekeza??? Maana mwenye nia na uwezo wa kuwekeza haitaji kua raia wa nchi anayofikiria kwenda kuwekeza bali jinsi gani anaweza kufaidika au kunufaika na uwekezaji wake.

    ReplyDelete
  4. Mbona hatumuoni huyo mdau,kuna error,kusema kweli Mimi sioni kitu,naona maoni tu kule chini.

    ReplyDelete
  5. Asante sana kwa kutuelimisha. Kweli inabidi kujipanga na vile vile kuisoma na kuielewa katiba yetu.

    ReplyDelete
  6. Nakumbuka miaka ile ya zamani kuna mama mmoja hapa Zanzibar alikana uraia wetu na kuchukua uraia wa Ughaibuni. Siku anarudi zake Ughaibuni baada kumaliza holiday yake pale uwanja wa ndege Zanzibar aligoma kutoa airport charge kama foreigner na kudai kuwa yeye ni mzaliwa wa Zanzibar! Sote tulimshangaa huyu mama vipi wewe si una passport ya Ughaibuni kulikoni? Baada ya miaka kupita tukaja kujua kwamba kuwa na uraia wa Ughaibuni haina maana kuwa na pesa. Kumbe wengi wao hawa raia wa Ughaibuni huwa hawana pesa maana wapo wenye Unemployment Benefit huko Ughaibuni sasa hutafuta visababu kuwa wanataka uraia pacha ili wakwepe kodi zetu hapa.

    ReplyDelete
  7. Mdau aliyerusha video ya kuhusu swala la Diaspora, aligusia kuhusu TITLE DEED. Asilimia kubwa sana ya Ardhi za vijijini hazina Title Deed.
    Ardhi yangu iko kijijini na ni ya kuridhi kwa mila zetu.
    Swali: NINA URAIA WA NCHI NYENGINE NA NIMEPOTEZA URAIA WA TANZANIA BY DEFAULT. KWA MIMI KAMA MIMI SIJAWAHI KUUKANA URAI WA TANZANIA, ILA NIMENYANG'ANYWA BY DEFAULT. KWAHIYO NITANYANG'ANYWA URITHI WANGU KULE KIJIJINI KWANGU?

    ReplyDelete
  8. Sheria zote za nchi watu wanazijua. Tatizo sio kusomea watu sheria, tatizo ni waone kama hizo sheria zimepitwa na wakati na zina mapungufu na zinahitaji mabadiliko.

    Watu wameongea kama points tu kwamba haizewezekani mtanzania ambaye kazaliwa tanzania avuliwe uraia wake (sio kwa yeye kutaka bali kwa sheria iliyopitwa na wakati). Kama mtu aliamua kuandika barua kuukataa uraia kwa Tanzania ni swala jingine, ile hawa wamevuliwa bila kupenda. Haikuwa nia yao, ni kwa sababu tu za kibiashara wamelazimika kuchukua uraia wa nchi ingine ila sio kwamba hawapendi tanzania.

    Watu wanahitaji mabadiliko ya sheria na katiba, kwa sababu hakuna mtanzania anayependa kuvunja sheria.

    Sisi watanzania tulio nje ya nchi utakuta ni wazalendo zaidi kuliko hata walio ndani maana sisi hatuwezi hata kuiibia nchi yetu kwa jinsi tunavyoipenda na junsi tunavoisaidia hata sasa kupitia Diaspora.

    Labda tukuelimishe kwamba uraia pacha utatusaidia kufanya biashara nje ya nchi kirahisi, kusafiri nchi mbali mbali na passport ya tanzania kuna mlolongo mrefu wa kuomba visa na kukataliwa hivo biashara zetu zinasimama. Uraia kama wa nchi za dunia kwanza utakuwezesha kuokoa mda mwingi kwenye biashara, kuingia na kutoka nchi za nje kwa biashara.

    Kingine, uraia pacha unasaidia watanzania wenzako kulipa pesa ndogo kwenye shule za nje na huduma nyingi kubwa za nje ya nchi ambazo kama tunajua nyie mlio nyumbani umekuwa mkilalamika matumizi makubwa wa viongozi kwenye hospitali za nje. Kama unafahamu Raisi kapiga marufuku safari hizi kwa sababu matumizi makubwa. Ila wenye uraia pacha wanatibiwa bure nchi hizi au kwa pesa ndogo sana hivo inawasaidia kimaisha na kuwapunguzia mzigo wa kifedha. Labda kama useme hili La mtanzania nwenzako kupata benefits hizi linakukera.

    Watanzania walioko nje ya nchi kwa taarifa yako hawana hata haja ya kazi za serikali au kuingia kwenye siasa tanzania. Nia yao ni kunufaika kibiashara kwa uraia pacha ili watulie hizi pesa nchini Tanzania kuleta maendelea na manufaa kwa kufungua biashara kama wazaelendo.

    Mwisho, uraia pacha utawezesha serikali kukusanya mapato hata kwa watanzania walio nje ya nchi kuchangia shuguli za maendeleo. Sasa hivi huwezi kumchangisha mtu au kumpa sheria hiyo atoe kodi wakati hata humtambui kama mtanzania. Hivo inayokosa manufaa ni Tanzania kwa ujumla na Mtanzania mwenzako unamuwekea ugumu usio na lazima.

    Tufunguke mawazo sasa, sote tunaipenda tanzania hivo wala msituelewe vibaya. Sisi tukifanikiwa na nyie mnafanikiwa maana biashara tunazoanzisha zina ajiri ndugu zako na pesa za kodi zitajenga barabara, hospitali nk ili hata wewe unayesoma email hii upate nafuu ya kulipa kodi. Yaani kila mtanzania ndani na nje ya nchi achangie maendeleo ya nchi yetu.

    Hili ni jambo la maendeleo ungeni mkono uraia pacha bungeni nchi yetu ipige hatua tuache siasa sasa maana siasa zinawagawanya wananchi na kuleta mifarakano bila maendeleo. Kenya, South Africa na nchi nyingi za africa zina uraia pacha na tazameni pesa zinavoingia. Uzalendo sio kukaa tanzania miaka yote tu, nakuwagomea wengine maendeleo kisa tu wanatumia uraia pacha kibiashara, mzalendo ni yule aliye tayari kuitumikia nchi yake popote alipo akihitajika na nchi yake, kwa ajili ya nchi yake.

    ReplyDelete
  9. Pia tukumbuke ya kuwa watanzania wengi hizi mali wamezipata kabla hawajaenda nje ya nchi, ni mali zao, wamefanya kazi na hawajamwibia mtu.

    Kama marekani, UK, Australia, na nchi kubwa na tajiri zinakubali uraia pacha kwa sababu wanachukukua kodi ndani na nje ya nchi, sisi Tanzania nchi maskini tunataka kukuwa ndo tunakuwa wajeuri mpaka basi kwa sheria za miaka ya 70 zinahitaji mapendekezo mapya. Sisi tuliotoka nje tunajaribu kuwasaidia kimawazo mnaona sasa tumekuwa adui.

    Kweli tunawaona nyie mliokuwa wazalendo zaidi na vyeti feki, mmeibiwa na mafisadi bado mnachekelea, huduma za afya vijijini mbovu, hakuna uwazi wa matumizi ya pesa, chuoni wanafunzi wanapata mokopo kwa tabu. Yet mnaona huo ndo uzalendo kuliko yule aliyeamua kutafuta urahisi wa biashara na kazi nje ya nchi ili kukupunguzia wewe changamoto na kukupa nafasi moja ya wewe kuto kuwa na competition nyumbani ya kazi. Kweli nyie kiboko.

    Tunakataa kodi ya bure ya mtanzania ambayo ingeingia kukusaidia unchumi. Mnasema hatuna hela wakati diaspora inatuma dola milion 225 kwa mwaka. Na hiyo ni kwa hayari sio kwa sheria.

    Kweli Hatuna upendo wa kuwalinda watanzania wenzetu walio nje ya nchi tunasingizia sheria ambazo zimetungwa na binadamu na zinaweza kubadilishwa kukidhi haja za watanzania walio ndani na nje ya nchi.

    Ama kweli Tanzania tunatia fora kwa kufungwa kimawazo kwa kuto takiana maendeleo binafsi na maendeleo ya nchi nzima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...