Meneja wa TANROADS mkoa wa
Shinyanga Mhandisi Wittonde Philipo ameelezea utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya barabara mkoani mwake na kueleza kwamba maendeleo ya miradi mkoani mwake ni mazuri.
Akiongea na Afisa habari wa
TANROADS Bi. Aisha Malima, Mhandisi Phillipo alisema kuwa miradi miwili ipo
katika hatua za kati na mwisho katika utekelezaji wake.
Miongoni mwa miradi
iliyotembelewa na Afisa Habari huyo na
ujumbe wake ni barabara ya Mwigumbi – Maswa yenye kilometa 50.30 inayounganisha mkoa wa Shinyanga na
Simiyu.Kwa upande wa mkoa wa Shinyanga ni kilometa 16 na kilometa 34 mkoa wa
Simiyu.
Mradi huu umeanza mwaka jana
mwezi wa sita na matarajio ni kumaliza Aprili
mwaka ujao. Utekelezaji wa mradi huu ambapo kwa sasa ni asilimia 65
unasimamiwa na Kampuni ya Mkandarasi ya CHICO kutoka China pamoja na Wahandisi Washauri wa Kampuni ya KYONDONG Engineering Co. Ltd kutoka Korea ya
Kusini, JV CORE Consulting PLC ya
Ethopia, LUPTA Consults Ltd ya Tanzania na ACE Consultants kwa gharama ya
shilling billioni 61.461 na inafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya
Tanzania.
Mhandisi Wittonde Phillipo
alielezea changamoto kadha zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa barabara hizo kuwa
ni ukosefu wa maji kwa ajili ya kazi ya ujenzi. Aidha wakati wa masika
mkandarasi aliweka jitihada ya kuchimba mabwawa kuhakikisha kazi haisimami
kutokana na ukosefu wa maji.
Changamoto nyingine ilikuwa
eneo la kujenga barabara ambapo alitumia
fursa kuwashukuru wananchi walio toa ushirikiano wa kutosha na walio vunja
nyumba zao bila ya matatizo yeyote.
Mhandisi Phillipo alieleza
kwamba barabara hii inaendelea vizuri na kwa sasa mkoa wa Shinyanga una miradi
mingi ambayo imekamilika kwa kiwango cha
lami .
Meneja wa Mkoa wa TANROADS Shinyanga (katikati) akipewa maelezo juu ya ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa (km 50.30) na Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Kikandarasi ya KYONGDONG Engineering Co. Ltd ndugu Kim Hyung Gyu
Ndugu Kim Hyung Gyu – Mhandisi Mshauri akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya kitaifa wa Mwigumbi – Maswa (km 50.30) kwa Meneja wa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Augustino Wittonde Phillipo.
Kazi za ujenzi katika barabara ya Mwigumbi – Maswa (km 50.30) zikiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...