Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, (UCSAF), Joseph Kilongola, (wakwanza kushoto-mbele), Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mhandisi Peter Ulanga, (wakwanza kushoto-nyuma), wakishuhudia Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, (mwenye tai nyekundu), Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (wakwanza kulia), Diwani wa Kata ya Bwilingu, Lucas Lufunga, (wane kulia), na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Edes P.Lukoa, wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya kopyuta zilizotolewa na UCSAF kwa shule ya Sekondari Chalinze mkoani Pwani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga, akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, (anayeshughulikia mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwaasa wanafunzi kujifunza zaidi elimu ya kompyuta na sio kujifunza word, excel na access, kwa sasa mafunzo hayo hayatoshi, na hivyo aliwahimiza wanafunzi lkujifunza zaidi ya hapo na hususan kutengeneza nyenzo za kutumia kompyuta, (computer applications).

"Wenzetu huko nchi za nje ambako wametutangulia katika teknolojia hii ya mawasiliano ya kompyuta, tangu shule za vidudu watoto wanafundishwa jinsi ya kuandika programs, bila shaka sisi sote wenye simu za mikononi kwenye simu zetu tunazo nyenzo mbalimbali (applications),  tunazozi zitumia kupakua (dowload), vitu mbalimbali  kutoka Google play, kwa hivyo ni vema tukaanza kujiongeza ili kupata manufaa zaidi ya kompyuta." Alisema Profesa Kamuzora.

Mbunge wa chalinze, Ridhwani Kikwete, aliushukuru mfuko wa UCSAF kwa msaada huo kwani utasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa kompyuta shuleni hapo. "Naamini msaada huu utatusaidia sana kuhakikisha wananfunzi wetu wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia internet lakini pia kujiongezea maarifa mbalimbali yatokanayo na kompyuta.

 Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (aliyesimama), akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea msaada wa kompyuta hizo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Edes P.Lukoa.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MFUKO wa Mawasiliano kwa wote, (UCSAF), umetoa msaada wa kompyuta 10 kwa Shule ya Sekondari Chalinze mkoani Pwani ikiwa ni moja ya jitihada za Mfuko huo kuwawezesha wananchi wa kada mbalimbali kupata fursa ya mawasiliano.

Akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi ya msaada huo, shuleni hapo mwishoni mwa wiki, mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola alisema, mfuko ulipokea maombi kutoka shule hiyo ya uhitaji wa kompyuta ili kuwawezesha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hiyo kupata fursa ya kujifunza teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta. 
 
"Ili kuwafundisha watoto wetu kupitia internet, ni vizuri shule iwe na kompyuta za kutosha, Mfuko ulikubali ombi la shule ili kuwapatia kompyuta 10  kuiwezesha maabara yao ya kompyuta kutumika kwa ufanisi zaidi, na ni matumaini yetu kuwa kompyuta hizi zitatumika kwa malengo .

yaliyokusudiwa katika kuwaelimisha wananfunzi na kuwawezesha walimu kuzitumia kama nyenzo ya kupata maarifa ya ziada kwa ajili ya kufundisha na hivyo kuboresha maendeleo ya wananfunzi na jamii inayotuzunguka." Alisema na kuongeza.
 Baadhi ya kompyuta zilizotolewa na Mfuko kwa shule hiyo

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...