Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua kiuchumi.
Dkt.Possi ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule zenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye ulewavu cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) na Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto nyingi za watu wenye ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha watu hao katika mipango yote ya maendeleo.

“Halmashauri ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa hawawezi” .Alisema Mhe.Possi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu (hawapo pichani) na watendaji wa Serikali juu ya umuhimu wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli za maendelea wakati wa ziara yake Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma Novemba, 2016.
 Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao alipotembelea kituo cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action(PEDIPA) wakati wa ziara yake Peramiho. 
 Mhazini wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) Mwl.Elswida Charles akimkabidhi risala ya kikundi hicho kwa  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi Peramiho Ruvuma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi   akimkabidhi Mwenyekiti wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo Kiti Mwendo ili kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...