THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MIchuano ya SHIWATA yaanzaBENDI saba za muziki wa dansi zimethibitisha kushiriki mashindano ya Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) na timu nane za soka za maveterani nazo kumekubali kumtafuta bingwa wa mchezo huo.


Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa mashindano hayo ambayo yanashirikisha michezo jingine ya mpira wa kikapu,Sarakasi,kun-fu na kaswida,mshindi wa kila mchezo atakabidhiwa zawadi katika kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga kwenye  sherehe za kugawa  nyumba Desemba mwaka huu.

Taalib alisema mashindano ya soka yatafanyika Desemba 9 mwaka huu kwenye viwanja cha shule ya Msingi Kitunda zikipambana timu za Kisarawe veterani, Stakishari veterani, Vituka veterani, Mbagala veterani, Kigogo TZF, TBC veteran na wenyeji Kitunda na Kivule veteran.

Alisema katika muziki wa dansi bendi zilizothibitisha kushiriki ni Tanzania One Theatre (TOT), Magereza Jazz (Mkote Ngoma), Mwenge Jazz (Panselepa),
Hisia Sound (Abdul Salvador) JKT Kimbunga Stereo,Vijana Jazz na Wazee Sugu ya King Kikii ambazo zitaoneshana umahiri wao kwenye kuimba na kupiga vyombo.

"Mpaka sasa mashindano ya Kikapu yanayoshirikisha timu 16 za wanaume na nne za wanawake yanaendelea viwanja vya ndani vya taifa.Timu hizo ni Kurasini Meat,Yellow Jackets,Chui,Kijichi Worriors,Segerea BC, Jogoo,TMK Rockets,Oilers, Hopper,  TM Rockets, Chang'ombe,Montfort,"Timu za wanawake ni Ukonga Queens,Vijana Queens,Ukonga Princesses na Oilers Princesses ambazo  bingwa atazawadiwa kikombe na kukabidhiwa Kiwanja cha kujenga ofisi ya timu"alisema Taalib.

Alisema katika mashindano ya kun-fu klabu zilizothibitisha kushiriki ni Begeja wu --shu, Karakata Wu-shu na Kigogo Wu-shu ambazo zitapambana kwenye ujumbe as CCM Mchikichini kwa mchezaji mmoja mmoja.
Naye msimamizi wa mchezo as  sarakasi,Selemani Penne alisema maandalizi ya  mashindano ya mchezo huo yamekamilika na itavukutanisha vikundi vya Butterfly Arts Group,Happy Center acrobatic, Black Lion na Jivunie.