Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imesaini mikataba 06 yenye thamani ya shilling milioni 579.8 na wakandarasi 06 tofauti kwa lengo la kufanya  matengenezo  ya barabara mbalimbali za halmashauri zenye jumla ya Km 70 zilizopo kwenye kata na vijiji  vya halmshauri hiyo .

Taarifa ya  kitengo cha habari na mwasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imezitaja barabara zinazotarajiwa kufanyiwa matengenezo wakati wowote kuanzia sasa kuwa  ni pamoja na barabara ya Mdabulo- Lulanda kwa urefu wa km 9.0, barabara ya Mninga – Mkalala – Kasanga km 9.0, barabara ya Tambalang’ombe – katwanga km 10.
Barabara nyingine ni  barabara ya Vikula – kilosa Mufindi km 12, barabara ya Lutheran – Isupilo km 7.5 huku ile ya mtili- ifwagi mpaka Mkuta ikifanyiwa matengenezo kwa km 13.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakati wa hafla fupi ya utiaji hihi wa  mikataba hiyo kati ya Halmashauri na wakandarasi waliopewa kazi ya matengenezo hayo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA amewataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia vigezo vilivyo kubalika kwenye kandarasi walizozisaini ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa wakati, kuzingatia ubora utakaoendana na thamani ya Fedha watakazo lipwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. RIZIKI SHEMDOE amesema kuanzia sasa ofisi yake   itakuwa ikisaini mikataba yote kwa uwazi na akawatoa hofu wakandarasi hao kwa kuahidi kulipa Fedha zao kwa wakati mara tu watakapokamilisha kazi zao.
Mwenyekiti wa halmshauri FESTO MGINA akikabidhi mkataba kwa mmoja wa wakandarasi huku Mkurugenzi Dkt. RIZIKI SHEMDOE akishuhudia.
Mkurugenzi Dkt RIZIKI SHEMDOE akisani kandarasi hizo kama mtendaji Mkuu wa halmashauri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...