Mkandarasi anayejenga barabara ya Magole - Turiani (ChinaCivil Engineering Construction Corparation-CCECC) ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo mapema, lakini ameiomba serekali imuunge mkono kwa kutoa fedha kwa wakati.

Katibu Mkuu wa Asasi ya Urafiki wa Tanzania na China, Bwana Joseph Kahama,  amewambia waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana kuwa  siku za nyuma serekali imekuwa ikichelewa kutoa  fedha za ujenzi wa maradi na ujenzi umekuwa ukisimama mara kwa mara. Hata hivyo Kahama  amesema ana matumaini makubwa ya  ujenzi kukamilika  katika muda muafaka kwani kuna mawasilianao ya mara  kwa mara kati yao  na TanRoads.

Serekali tayari imetoa  bilioni 41.8, kati ya bilioni 66.7 ambazo zinatarajiwa kujenga barabara hii.

Kahama amesema kuwa hakuna tarehe mpya ya kukamilisha kazi ambayo pande mbili zimekubaliana. Lakini amesema wafanyakazi wana ari ya kazi na kuwa  mradi utakamilika mapema iwapo serekali itatoa fedha katika muda unaoruhusu ujenzi uendelee kwa kasi inayotakiwa.  Fedha ikichelewa, kasi ya ujenzi inavia na mradi unadorora, ameeleza.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Kabwe amekaririwa katika vyombo vya habari akimuhimiza mkandarasi kukamilisha kazi kabla au ifikapo Septemba 2017 na kwamba ujenzi usifike mwaka 2018.

Kahama amesama kwamba Dr Kabwe amejionea mwenyewe hali halisi ya ujenzi wa barabara na kuhakikishiwa na Mhandisi  Khatibu Khamis kwamba kazi itakamilika katika muda muafaka  kwani hakuna tatizo la vifaa au wafanyakazi.  Tanzania na China, ameeleza,  zina mawazo sawa juu ya maendeleo ya wananchi na uhusiano wa kuwepo barabara katika kasi ya wananchi kujiletea maendelo.

“Tunawasisitizia wenzetu jambo upatikanaji wa fedha mapema. Ujenzi wa barabara unaathiriwa na mambo mengi yasiyotarajiwa kama vile mvua kubwa au mafuriko.  Fedha isipotolewa kwa wakati, kuna hatari ya ujenzi kukwama,” amesisitiza Kahama.

Barabara ya  Mikumi-Mzina inaunganisha Mkoa wa  Tanga  na Mikoa ya  Morogoro na Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...