Mke wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika
wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam
ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo tarehe 11 Novemba, 2016 baada ya afya yake
kuimarika.
Kabla ya kuondoka
katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru
Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri
aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.
"Namshukuru
sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na
Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina
fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani
nikiwa na afya imara.
"Naomba pia
niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri
na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu
yangu" amesema Mama Janeth Magufuli.
Mama Janeth
Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi tarehe 09 Novemba, 2016 baada ya
kuugua ghafla na kupoteza fahamu.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
11 Novemba,
2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa
anatoka kwenye Wodi ya Sewahaji katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kurejea nyumbani mara baada ya kuruhusiwa baada ya kupata
nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 9
Novemba 2016.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru
Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru
Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea
nyumbani mara baada ya kupata nafuu. Picha
na IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...