THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO MHANDISI FELCHESMI MRAMBA, ATEMBELEA VITUO VIPYA VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VYA JIJINI DAR ES SALAAM


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea vituo vitatu vipya vya kupooza na kusambaza umeme vilivyo kwenye mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.

Vituo alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha Ilala Mchikichini.

Kwa takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali ya juu.

“Nimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya kubadilisha miundombinu yetu ya umeme, wakazi wa jiji la Dar es Salaam, sasa watapata umeme wa uhakika na ulio na ubora wa hali ya juu, jambo la kufurahisha sana ni kwamba mabadiliko haya yamekwenda sambamba na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda, bila shaka umeme huu utawezesha kufikia azma hiyo ya serikali.” Alisema Mhandisi Mramba, baada ya kukagua kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha katikati ya jiji.
Mhandisi Mramba alisema, nia ya TANESCO ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya kukatika umeme mara kwa mara au kupata umeme hafifu usio na nguvu. “Mmeona mitambo hii nimipya kabisa nay a kisasa inayotumia teknolojia ya kisasa.” Alitoa hakikisho.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam