THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KINYEREZI II

NA K-VIS BLOG/KAHLFAN SAID

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (anayezungumza pichani), amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II utakaozalisha umeme wa Megawati 240 unaotekelezwa na shirika hilo jijini Dares Salaam.

Mradi huo ulizinduliwa Machi 2016 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kuweka jiwe la msingi ambapo eneo hilo lilikuwa pori tu kazi ya kusafisha eneo ili kuanza ujenzi ilianza mieziminane iliyopita.

“Kwa wale waliokuwepo siku Mheshimiwa Rais anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huu, mtakumbuka kuwa eneo lote hili lilikuwa pori, napenda niwapongeze wahandisina mafundiwote mnaotekeleza ujenzi huu kwa kazi nzuri nakasi ya kuridhisha.” Alipongeza Mhandisi Mramba, ambaye alitembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki kukagua maendeleoyaujenzi wake.

Wahandisi wa TANESCO wakishirikiana na wenzao kutoka SUMITOMO CORPORATION NA TOSHIBA za Japan na washauri wa mradi Lahmeyer International ya Humburg nchini Ujerumani, ndio wanaojenga mitambo hiyo kwa ambapo unatekelezwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania na Japan.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo, Meneja Mradi, Mhandisi Stephen Manda alisema ni pamoja na ujenzi wa msingi wa kitalu namba moja (Foundation Works Block I na ujenzi wa msingi watenki la kuhifadhia maji (raw water tank).

“Kazi inaendelea vizuri napenda kukujulisha kuwa baadhi ya vifaa muhimu vimekwisha wasili na tunachosubiri pengine kufikia mwezi Januari ni kuwasili kwa mashine zenyewe (Turbines), hivi sasa tuko kwenye mazungumzo na watu wa TANROAD na mamlaka nyingine kuhusu utaratibu wa kusafirisha mitambo hiyo kutoka bandarini kuiletahapa.” Alifafanua Mhandisi Manda.

Akielezea zaidi kuhusu manufaa ya mradi huo pindi utakapokamilika, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhanidis Felchesmi Mramba alisema, TANESCO iliwaahidi watanzania kuwa kwa kushirikiana na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umeme ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme mwingi zaidi ili hatimaye uende sambamba na malengo ya serikali yaawamu ya Tano ambayo imedhamiria kujenga nchi ya viwanda.

“Nia yan Mheshimiwa rais ya kujenga nchi ya viwanda itafanikiwa kwa vile sasa umeme mwingi na wa uhakika utapatikana ili kuhudumia viwanda vilivyopo na vipyavinavyoendelea kujengwa.”Alihitimisha Mhandisi Mramba.
Mhandisi Mramba, (kulia), akiongozana na Meneja Mradi wa ujenzi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda.

Ujenzi wa msingi wa tenki la kuhifadhia maji (raw water tank).