THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA KITUO CHA HUDUMA SHIRIKISHI DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

Na George Binagi-GB Pazzo

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka maafisa ustawi wa jamii kwa kushirikiana na askari polisi kitengo cha dawati la jinsia, kufikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wananchi ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

Mongella ametoa agizo hilo wakati akifungua kituo cha huduma Shirikishi dhidi ya Ukatili wa kijinsia na watoto cha One Stop Centre kilichojengwa na taasisi ya Pact Tanzania kwa ufadhiri wa watu wa Marekani, katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Amesema hatua za kukabiliana na ukatili wa kijinsia zinapaswa kuchukuliwa mapema badala ya kusubiri utokee katika jamii ambapo amesema watakaokuwa wakipatikana na hatia za kujihusisha na ukatili wa aina hiyo watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sekour Toure, Dkt.Leonard Subi, amesema kituo hicho kitajumuisha watumishi mbalimbali ikiwemo polisi, maafisa ustawi wa jamii pamoja na wataalamu wa afya kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kinjinsia ambavyo bado vimeshamiri mkoani Mwanza.

Amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba, wananchi 238 mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za ukatili wa kijinsia katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya na kati ya hao 77 ni ukatili wa watoto. Kituo hicho tayari kimehudumia watu wazima 30 waliolengwa na ukatili wa kijinsia huku watoto wakiwa ni 67.

Naye Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi milioni 80 ikiwa ni pamoja na gharama za vifaa na mafunzo ambapo kinakuwa kituo cha nane nchini miongoni mwa vituo vya One Stop Centre.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure, hii leo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure.