Na Grace Singida 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameipongeza hospitali ya Kiomboi ambayo ni ya Wilaya ya Iramba kwa kupata hadhi ya nyota mbili kutoka sifuri na kuwahamasisha kuendelea kuboresha utendaji ili kupata hadhi ya nyota tatu.

Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ametoa pongezi hizo alipotembelea hospitali hiyo akiambatana na wageni kutoka shirika la Water Aid International ambalo limefadhili ukarabati wa miundombinu hospitalini hapo kwa shilingi milioni mia tano kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema hospitali ikiwa na hadhi ya nyota tatu itasaidiwa na serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuipatia wataalamu zaidi, kuboreshewa zaidi miundombinu, kuwekwa katika mipango ya kitaifa pamoja na kupata fedha zaidi.

Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa kutokana na kuboreka kwa huduma za hospitali ya Kiomboi wagonjwa wameongezeka sana na hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri ya Wilaya ya Iramba inaboresha Vituo vya Afya vya Mgongo na Ndago ili vituo huduma za zarudha za Mama na mototo kwa kufanya upasuaji na hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Kiomboi. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe akipata maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto mahututi (Neonatal Intensive care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba. 
Mwakilishi wa Shirika la Water Aid International akiangalia akinamama wanaosubiri kujifungua wakichota maji, miundombinu ya maji imekarabatiwa na shirika hilo wakishirikiana na shirika la SEMA Tanzania. 
Akina mama wanaosubiria kujifungua wakiwa nje ya wodi ya kusubiria iliyokarabatiwa kwa ufadhili wa shirika la Water Aid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...