THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA ATOA SIKU SABA UTEKELEZAJI WA MAADHIMIO YA WASANII WA FILAMU.


Na George Binagi-GB Pazzo

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, amemtaka Afisa Utamaduni mkoani mkoani hapa, kuhakikisha maadhimio yaliyoafikiwa na wasanii wa filamu mkoa wa Mwanza yanaanza hatua za utekelezaji ndani ya siku saba.

Nje ya hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Tesha amesema Afisa Utamaduni mkoa wa Mwanza, James Willium, kwa kushirikiana na maafisa utamaduni wa halmashauri zote za mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha wanatoa mikakati ya utekelezaji wa maadhimio yaliyotolewa kwenye mafunzo hayo ili utekelezaji huo uanze mara moja.

Miongoni mwa maadhimio saba ya wasanii walioshiriki mafunzo hayo ambayo yamewasilishwa na Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela, ni pamoja na uongozi (Serikali) wa mkoa wa Mwanza kusaidia upatikanaji wa kituo cha sanaa (studio ya kisasa) kwa ajili ya kurekodia filamu na vipindi vya runinga pamoja na kushirikishwa kwenye dhifa mbalimbali za kimkoa na kitaifa ili kuonesha kazi sanaa zao.

Katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa, ametoa bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40 kilichopo Nyegezi Jijini Mwanza ili wasanii wa filamu mkoani Mwanza wajengewe studio kwa ajili ya kurekodia kazi zao ambapo Mfuko wa Pensheni wa PPF umeonesha nia ya dhati ya kufadhiri ujenzi wake.

Zaidi ya washiriki 300 wamepata mafunzo hayo ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema yamelenga kuwajengea weledi wadau wa filamu wakiwemo waigizaji, waongozaji na wahariri, kutengeneza kazi zenye ubora, kutambua majukumu ya bodi hiyo, hakimili na hakishirikishi ili kukuza soko la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso (kulia), wakati wa ufungaji wa Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza yaliyoanza juzi Novemba 10 na kutamatika leo Novemba 12,2016 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mhe.Tesha amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani Mwanza, Ramadhan Mustapha (kushoto), akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.