Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dkt. Augustine Mrema  amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kasim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamalia wema baada ya kukidhi vigezo.

Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.

“Mimi nimeona nisinyamaze. Napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?. 

Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.

Dkt. Mrema ameweza kuonyesha nyaraka ikiwemo risiti mbalimbali walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema haki ya kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamalia wema walioweza kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.

Pia ameongeza kuwa,  mpaka sasa magereza mbalimbali kuna msongamano wa wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila hawajapata fedha za kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama Rwakatare wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.Hivi karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.

Awali ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni. 

Kwa mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya vyombo vya habari hapa mchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo na  kuongeza kuwa, wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao. 

Hata hivyo Mrema alisema  mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya Parole katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...