Hapa kazi tu ni kaulimbiu inayohamasisha watu kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia fursa mbalimbali zilizopo, usemi huu umetimia kwa Mama Paulina Kulwa mkazi wa Mwanza baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni mia moja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya CBA. 
Paulina alikabidhiwa hundi hiyo katika ofisi za Vodacom jijini mwanza na Meneja Masoko na huduma za Kifedha Vodacom Tanzania, Noel Mazoya na kusema lengo la kuanzisha huduma hii ni kuwasaidia Watanzania kuwa na utamaduni wa kuweka akiba. 
 Bi Paulina Kulwa (Kulia) akikabidhiwa hundi ya mfano wa Tsh Milioni 100 baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Jiongeze na M-Pawa
 Bi Paulina Kulwa (Kulia) akiwa na pacha wake katika duka la Vodacom City Mall jijini Mwanza katika hafla ya kumpongeza na kumkabidhi hundi baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Jiongeze na M-Pawa
Mshindi wa Jiongeze na Mpawa akiwa na maafisa toka Vodacom na CBA katika hafla fupi ya kumkabidhi mfano wa hundi na kumpongeza. Toka kushoto ni Ayubu Kalufya Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Meneja Masoko wa huduma za Kifedha wa Vodacom Noel Mazoya, mshindi wa milioni 100 Bi Paulina Kulwa, Solomoni Kawiche Mkuu wa masoko - CBA na Eric Luyangi Mkuu wa MPawa - CBA. Video ya hafla hii BOFYA CHINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...