Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk John Lwegasha akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuanza kwa uchunguzi na tiba ya homa ya INI (Hepatitis B) katika hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swani na Dk Eva Owisso wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swai akifafanua jambo kwenye mkutano huo leo.
“Hatua hiyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki katika udhibiti na tiba ya ugonjwa huo”
Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Disemba Mosi mwaka huu inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure ya  ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Rwanda katika udhibiti na kutoa tiba ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo, John Lwegasha amesema ni wakati muafaka wa watu kujitokeza na kupima afya zao kwa ujumla na kwa wale waliothirika na ugonjwa huo wajitokeze ili kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupata nafasi ya tiba kulingana na miongozo ya tiba inavyoelekeza.

“Utaratibu mwingine wa uchangiaji wa gharama za matibabu katika maeneo mengine ya uchunguzi na tiba ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa gharama za kumuona Daktari utabaki kama ulivyo,” amesema Dk. Lwegasha.

Tatizo la ugonjwa huo Tanzania, kwa mujibu wa Dk . Lwegasha inakadiriwa kuwa watu wanane kati ya watu mia moja wana maambukizi ya ugonjwa huo na kwamba kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya kile kinachokadiriwa kwenye maambukizi ya Ukimwi kitaifa ambacho ni asilimia pungufu ya sita.
“Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili asilimia 60 ya wagonjwa wanaokutwa na Saratani ya Ini mara nyingi imetokana na maambukizi ya virusi hivyo,” amesema Dk. Lwegasha.

Kuhusu tiba amesema kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi , ugonjwa huo sugu wa Homa ya Ini hauna tiba ya kuponya isipokua dawa zilizopatikana hadi sasa zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi mwilini na kuzuia madhara kwenye Ini.

Ugonjwa wa Homa ya Ini ( Hepatitis) unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na maambukizi yaugonjwa huo yanashahabiana na njia ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama , kuchangia sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...