Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeanza kambi maalumu ya upasuaji kwa watu wenye matatizo mbalimbali na watu zaidi ya wanane wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Upasuaji huo ambao unahusisha watu wazima na watoto unafanywa kwa ushirikiano kati ya Muhimbili, Tanzania Australia Society na Rafiki Surgical Mission.Timu ya madaktari wa MNH wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na watalaam hao ambao waliwasili nchini Novemba 19, 2016 kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo.

Watalaam hao wanne akiwamo daktari bingwa wa upasuaji, Dk. James Savundra jana walikutana na watalaam wa MNH wakingozwa na Dk Bingwa wa upasuaji Muhimbili, Edwin Mrema wamewafanyia uchunguzi wagonjwa na kuzungumza nao kabla ya shughuli hiyo kuanza.

Kwa mujibu wa Dk Mrema lengo ni kutoa huduma, kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani.Leo wataalam hao wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa watatu akiwamo mgonjwa aliyeathirika mkono wake baada ya kupata ajali ya moto.Upasuaji huo unahusisha wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ikiwamo walioathirika baada kuungua na moto, ajali na wenye uvimbe.
Dk Edwin Mrema (kushoto) wa Muhimbili na Dk. James Savundra kutoka Australia wakifanya upasuaji kwa mmoja wa wagonjwa leo. Kulia ni Sister Akiyo akishiriki katika shughuli hiyo. Mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji wa mkono baada ya kupata ajali ya moto.
Daktari bingwa, John Masago (kushoto) na Raymond Nkya (katikati) wote wa Muhimbili wakifanya upasuaji wa shingo kwa mmoja wa wagonjwa kwa kushirikiana na daktari bingwa kutoka Marekani, Mark Zafereo. Upasuaji huo unaofahamika kama RT MASTOIDECTOMY.
Dk Mawala Shabani (kulia) kutoka MNH akishirikiana na Dk Richard Wagner (kushoto) kutoka Marekani wakifanya upasuaji wa sikio kwa mmoja wa wagonjwa Leo. Upasuaji huo unafahamika RT MASTOIDECTOMY.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...