Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji kwa kutumia darubini (microvascular surgery) wa kuhamisha misuli na mishipa ya damu kutoka kwenye mguu kwenda sehemu nyingine chini ya mguu (free gracilis muscle transfer).

Upasuaji huu wa aina yake na ambao mara nyingi huchukua muda wa saa sita hadi saba una lengo la kujenga uwezo kwa watalaamu wa ndani ili waendelee kutoa huduma za ubingwa wa hali ya juu kwa Watanzania wengi zaidi na vilevile kupunguza kasi ya kupeleka wagonjwa nje.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye pia ameshiriki upasuaji huo Dk Ibrahim Mkoma amesema upasuaji huo unagharimu kiasi cha dola 40,000 za Marekani nchini Australia ikiwa ni gharama ya upasuaji tu.Lengo kubwa la ushirikiano wa upasuaji huu ni wataalamu kutoka Australia kuwaachia taaluma ya upasuaji huo madaktari MNH ili iweze kuendelea kufanya upasuaji huo mbeleni.

Aidha Dk Mkoma amesema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na utaratibu ambao utaanzishwa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, wa taaluma maalumu ya kusomea upasuaji wa aina hiyo ili kuweza kupata wataalamu zaidi kutoka nchini. Amesema hakuna chuo chochote Tanzania kinachotoa taaluma hiyo ya plastic surgery kwa sasa.

Dk Mkoma amesema MNH inajivunia kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Australia akiwapo Daktari bingwa James Savundra ambaye ni Rais wa Madaktari Bingwa wa upasuaji kutoka timu ya upasuaji nchini Australia.Daktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia, Dk James Savundra amesema upasuaji huo ni moja ya upasuaji ambao umekuwa ukifanyika kwa gharama kubwa.

Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Tanzania Australia Society na Rafiki Surgical Mission wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa kuvuna mishipa na misuli katika mguu wake wa kulia na kupandikiza katika sehemu yenye uhutaji husika. Madaktari bingwa wa Muhimbili wanaofanya upasuaji huo ni Dk. Ibrahimu Mkoma, Dk Edwin Mrema, Dk. John Tupa na Dk Frank Muhamba ambaye anapitia mafunzo ya kuwa daktari bingwa wa upasuaji. Mwingine ni daktari bingwa wa upasuaji, James Savundra na wataalamu wenzake kutoka Australia.
Daktari Bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Edwin Mrema akizungumza na waandishi wa habari Leo katika chumba cha upasuaji ambako kumefanyika upasuaji huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...