Kaimu Mkuu wa Idara ya Physiotherapy katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Christina Mgaya amemshukuru raia wa Oman, Nasr Al Jahadmy kwa kutoa msaada wa viti vya magurudumu matatu kwa ajili ya kubeba wagonjwa wakiwamo walemavu na waliopata kiarusi.

Mgaya amemuomba raia huyo kuendelea kuisaidia hospitali hiyo kwani kuna upungufu wa viti vya kubeba wagonjwa wakiwamo walemavu na waliopata kiarusi.

Msaada huo umetolewa leo na raia wa Oman, Nasr chini ya Taasisi ya Isqama iliyopo nchini Oman.

Msaada huo umetolewa kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wanaopata matibabu katika hospitali hiyo.

“Lengo ni kuwasaidia wagonjwa na pia tunatarajia kuleta misaada zaidi baadaye,” amesema Nasr.

Raia huyo ametoa msaada, huku Oman ikisheherekea sherehe ya kitaifa ya miaka 46 ya mfalme wa nchi hiyo, Qabous bin Said. Idara ya Physiotherapy inatoa huduma ya mazoezi ya viungo na mazoezi ya viungo kwa vitendo.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Physiotherapy katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Christina Mgaya (kushoto) akipokea msaada wa viti 10 vya magurudumu matatu kutoka kwa raia wa Oman, Nasr Al Jahadmy ambaye ametoa msaada kwa ajili ya kubeba wagonjwa waliopata kiarusi na walemavu. Katikati ni Mjumbe wa Baraza la Ulama BAKWATA, Sheikh Ally Khamisi na wengine ni wafanyakazi wa idara hiyo.
Mmoja wa kina mama waliofika Muhimbili Leo kupatiwa matibabu akiomba msaada wa kiti kutoka kwa Nasr Al Jahadmy kwa ajili ya kumbeba mtoto wake. Nasri ameahidi kumsadia mtoto huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...