Siku ya Kisukari Duniani- Muhimbili Yawapima Kisukari Wafanyakazi Wake LEO Na Neema Mwangomo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo imeadhimisha siku ya kisukari duniani kwa kuwapima kisukari wafanyakazi wa hospitali hiyo. 
 Leo wafanyakazi wa hospitali hiyo walikuwa wakipimwa kisukari na uzito pamoja na kupatiwa ushauri jinsi ya kupunguza uzito kwa wale waliobainika kuwa na uzito mkubwa. Wafaanyakazi waliojitokeza leo ni madaktari, wafanyakazi kurugenzi za utawala, wauguzi na wanafanyakazi mbalimbali wa hospitali hiyo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawurence Museru alikuwa mstari wa mbele katika kuwashawishi wafanyakazi kupima kisukari. 
 Naye Mkuu wa Kitengo cha Kisukari, Dk Mohamed J. Mohamed amesema Muhimbili imeona kuna umuhimu wa kupima kisukari kwa wafanyakazi wake kutokana na kubanwa na shughuli mbalimbali na hivyo mara nyingi wamekuwa wakikosa nafasi ya kupata huduma za afya. 
 “Tumeona ipo haja ya kutoa huduma hii kwani kuwa mfanyakazi wa Muhimbili haimaanishi kwamba upo salama kiafya hivyo tunafanya hivi ili wapate nafasi ya kupia kisukari,” amesema Dk Mohamed.
 Dk Elias Mwandwani akimpima kisukari mmoja wa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwa amevaa beji ikiwa ni ishara ya kuwamasisha wafanyakazi wa hospitali hiyo kupima kisukari leo
 Juma Selemani akipima uzito Leo kabla ya kupima kisukari  katika Hospitali  hiyo leo.
 Dk Faraja Chiwanga wa Muhimbili akimpima kisukari Juma Selemani katika hospitali hiyo Leo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni, ‘Kuwa Makini na Kisukari Pima Kujikinga.’ Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...