Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Muwada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma ukiwa na lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma kamili.

Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema hay oleo Bungeni Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada huo, huku akisisitiza kuwa una sehemu kuu nane ambazo zinaufanya kuleta mageuzi katika tasnia ya habari nchini na kuifanya kuwa taaluma kamili itayowaletea heshima wanahabari na tasnia hiyo kwa ujumla. 

“Hatuwezi kwa na vyombo vya habari makini kama hatutakuwa na wanahabari wenye taaluma ya habari nchini” alisema Nape.

Katika kuonesha ushirikishwaji wa wadau katika kutoa maoni yaliyolenga kuboresha Muswada huo, Waziri Nape amesema kuwa kumekuwa na ushirikishwaji mkubwa wenye wigo mpana kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja, wanataaluma wa habari, wanasheria kupitia Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA-TAN).

Wadau wengine walitoa maoni yao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Sikika, Wabunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na michango ya Wabunge kupitia Kamati nyingine ambao umesaidia katika kuboresha Muswada huo wenye dhamira ya kuleta ufanisi katika sekta ya habari. 

Miongoni mwa maeneo ambayo wadau hao wameyafanyia maboresho ili Muswada uwe na tija ni pamoja na kuainisha haki na wajibu wa wananhabari ikiwemo uhuru wa kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari pamoja na kuainisha haki ya chombo cha habari kukata rufaa kwa kuzingatia mfumo wa wazi na wa kidemokrasia kupitia vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama huku Jaji Mkuu akiweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kwa kesi za masuala ya kihabari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...