Diwani wa kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Shirika la Eguality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele na kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye (kulia),  akitoa taarifa fupi kuhusu kampeni hiyo  mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele, Diwani wa kata hiyo, Joseph Ngowa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye (kushoto), akipeana mkono na mgeni rasmi baada ya kumkabidhi risala.
 Mjumbe wa Soko la Mchikichini, Victor Kalokola akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Msaidizi  wa kisheria masokoni, Irene Daniel akitoa ushuhuda wa hatua zilizochukuliwa kwa baadhi ya watu waliobainika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Soko la Tabata Muslim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Diwani ana mamlaka gani kisheria kumfutia mtu leseni ya biashara? Labda kama mwandishi anamaanisha kibali cha kufanya biashara ndani ya soko hilo. Waandishi tuwe makini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...