THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MWAKILISHI WA SHIRIKA LA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA (UNDP) ATEMBELEA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZIMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimkabidhi Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015, Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson, wakati kiongozi huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto katikati) akimueleza jambo mgeni wake ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.
Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (hayupo pichani) wakati alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kulia kwake ni Mtathmini wa Mradi wa Shirika hilo, Consolata Sulley.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (hayupo pichani) Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ambayo pia alimkabidhi mgeni wake alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile akimueleza jambo Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson wakati alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kaimu Naibu Katibu wa Tume, Idara ya Uendeshaji Uchaguzi, Adam Nyando.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mary Longway (kushoto) akitoa shukrani kwa Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) ambaye ametembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto katikati ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mst. Damian Lubuva na wa pili kulia ni Mtathmini wa UNDP, Consolata Sulley. Picha na Hussein Makame, NEC